Hatuna kesi FIFA - Kamwe - EDUSPORTSTZ

Latest

Hatuna kesi FIFA - Kamwe

Hatuna kesi FIFA - Kamwe


Michuano ya EURO 2024 inaendelea leo mechi za kibabe zitapigwa leo usikose kuzitazama mechi hizi zote live buree kwenye simu yako download app yetu kutazama mechi zote live bure pia kwenye app hii kuna muvi zilizotafsiriwa kwa kiswahili pamoja na chanel za Azam tv na Dstv kudownload app hii bonyeza 👉🏻👉🏻HAPA

Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema klabu hiyo haina kesi yoyote FIFA baada ya kumalizana na wachezaji waliokuwa wana madai

Kamwe amesema tayari klabu imepokea taarifa ya uthibitisho kutoka FIFA kuhusu kukamilisha kwa madai ya wachezaji Mamadou Doumbia na Lazarus Kambole

"Tarehe 14 Juni, yaani siku moja kabla ya dirisha la usajili kufunguliwa, tulifanya malipo ya madai yote tuliyokuwa tunadaiwa na wachezaji FIFA"

"Kiufupi ni kwamba hatuna kesi yoyote ya madai kutoka kwa mchezaji yeyote FIFA. Tumekamilisha malipo ya Kambole na hata FIFA wenyewe wamethibitisha"

"Tatizo lililotokea ni mchezaji mwenyewe (Kambole) hajaingia katika mfumo wa FIFA kuthibitisha kupokea malipo hayo. Hivyo FIFA wametoa siku tano kwa mchezaji huyo kuthibitisha na kifungo kitaondolewa," alisema Kamwe

Akizungumzia mchezaji Augustine Okrah, Kamwe amesema klabu itatoa taarifa kuhusu mchezaji huyo pale wakati utakapofika

Kamwe amesema taarifa za usajili wa Yanga zitaanza kutolewa Julai 01 pale michakato yote itakapokuwa imekamilika

"Tutaanza kutoa taarifa za usajili Julai 01, kuna wachezaji tumewasajili lakini mpaka sasa timu zao za zamani hazijawapa barua za 'release'. Yaani wachezaji wamemaliza mikataba lakini hawataki kuwapa barua"

"Hivyo tunasubiri kukamilika kwa taratibu zote muhimu kabla ya kuanza kutangaza taarifa zao," aliongeza Kamwe



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz