Klabu ya Simba imefunguka kuhusu usajili wa kiungo mkabaji wa Singida Fountain Gate, Yusuph kagoma mzaliwa wa mkoa wa Kigoma ambaye amekuwa na msimu bora na kuwavutia matajiri wa Kariakoo.
Hayo yamesemwa na Meneja wa Idara ya Habari na Mawasliano wa Simba, Ahmed Ally kupitia Wasafi FM wakati akihojiwa kuhusu usajili wa mchezaji huyo ambaye anatajwa kumalizana na Yanga huku Simba nao wakiweka mkwanja mrefu kunasa saini yake.
"Yusuph Kagoma ni mchezaji mzuri, Ni mchezaji wa maana sana, sisi tuliwapoteza Jonas Mkude na Thadeo Lwanga, kwa hiyo kama tutampata Wanasimba tutafurahi sana kwa sababu tutaenda kutibu tatizo letu. Lakini hadi hivi sasa ninavyoongea, Kagoma ni Mali ya Singida F," amesema Ahmed Ally.
Post a Comment