Kocha Mkuu wa Yanga Migel Gamondi huwenda hatakuwa sehemu ya benchi la ufundi la Wananchi kwani mpaka sasa hajasaini mkataba mpya.
Gamomdi ambaye ameshinda ubingwa wa Ligi Kuu Bara pamoja na CRDB Federation Cup, amethibitisha kuwa mkataba wake umeisha jana na atafanya mazungumzo na Yanga kuona anasalia au la.
"Mkataba wangu na Yanga umeisha leo (jana) hivyo nitafanya mazungumzo na uongozi kuona taratibu za mkataba mpya," alisema Gamondi mara baada ya kushinda mechi ya fainali ya CRDB dhidi ya Azam FC kwa mikwaju ya penalti.
Licha ya kuwa haijajulikana kama atashawishiwa na ofa ya Yanga au la, Gamondi amekuwa akiwindwa na vilabu mbalimbali vikubwa hususan vya Afrika Kusini hasa baada ya kuonesha uwezo mkubwa kweye mechi ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita.
Post a Comment