Eng. Hersi: Tumekamilisha usajili wote, kazi kwako Ally Kamwe kutangaza - EDUSPORTSTZ

Latest

Eng. Hersi: Tumekamilisha usajili wote, kazi kwako Ally Kamwe kutangaza

Eng. Hersi: Tumekamilisha usajili wote, kazi kwako Ally Kamwe kutangaza

Mechi za EURO 2024 zinaendelea leo pia mechi za kirafiki nyingi zinapigwa leo usikose kuzitazama mechi zote live bure kwenye simu yako download app yetu kutazama mechi zote bure pia ukiwa na app yetu utaweza kutazama muvi zilizotafsiriwa kwa kiswahili pia utaweza kutazama chanel za Azam TV bure kudownload app yetu bonyeza 👉🏻HAPA kama utashindwa kudownload app jiunge na group letu la telegram upewe app kujiunga bonyeza HAPA

Eng. Hersi Said

Wakati uongozi wa klabu ya Yanga ukijiandaa kumuongezea mkataba kiungo mshambuliaji wake Pacome Zouzoua, umetangaza kukamilisha na kufunga usajili wake msimu huu na sasa wanasubiri kuwatangaza rasmi wachezaji wote waliowasajili.

Rais wa Klabu hiyo, Hersi Said amesema jana kuwa tayari wameshamaliza usajili na sasa vimebaki vitu vichache ikiwemo Idara ya Habari kuweka utaratibu ili waanze kuwaweka hadharani.

"Tupo makini, kazi kubwa tumeshaifanya, tumeshasajili na karibuni asilima 99 kazi imekwisha, hivi sasa tumeiachia tu Idara ya Habari kutengeneza njia nzuri ya kutambulisha wachezaji wote tuliowasajili," alisema Hersi.

Alisema katika usajili wao wamejikita tu kwenye maeneo ambayo wanaona yana mapungufu na si vinginevyo.

"Suala la usajili huu ndiyo wakati wake na ni muhimu sana kuliko wakati mwingine wowote, ni kipindi cha kutuliza akili ili kupata wachezaji wazuri.

"Sisi Yanga kuna maeneo ambayo tumelazimika kuyaboresha kwenye kikosi chetu ili kuwa bora zaidi, kwa hiyo nichukue fursa hii kuwaambia wana Yanga wawe tayari kuanzia tarehe moja Julai tutaanza kuelezea, au kutoa taarifa za usajili za wachezaji wetu wapya, wale tunaowaongezea mikataba na tutakaowaacha," alisema Hersi.

Wachezaji wanaohusishwa kutua kwenye klabu hiyo ni Wakongomani watatu, beki wa kushoto, Chadrack Boka kutoka FC Lupopo, kiungo mkabaji, Agee Basiala wa klabu ya Maniema Union na winga Emmanuel Lobota anayeichezea Singida Black Stars.


Mchezaji mwingine anayetajwa ni Chikamso Okechukwu, beki wa kati kutoka klabu ya Enyimba.

Wakati huo huo, klabu hiyo imesema ipo kwenye mazungumzo ya kumuongeza mkataba kiungo mshambuliaji, Pacome raia wa Ivory Coast ambaye kwa siku za karibuni amekuwa akihusishwa kutimkia klabu za FAR Rabat ya Morocco na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.

Ingawa Pacome ana mkataba wa mwaka mmoja zaidi wameamua kukaa naye ili wampe mkataba mwingine ili kuhakikisha anasalia kwa muda mrefu ndani ya timu hiyo.



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz