Mabosi moja ya klabu kubwa kutoka hapa Tanzania wapo mbioni kukamilisha dili la kumsajili aliyekuwa mshambuliaji wa AZAM FC, Prince Dube ambaye katikati ya msimu alijivunjia mkataba na klabu yake, huku ikielezwa kwamba anahitajika na miamba hao.
Prince Dube na Azam FC ilifikia hatua ya kufikishana hadi Kamati ya Haki za Wachezaji kwenye Shirikisho la Mpira wa Miguu TFF, ili kusikilizwa madai ya kimkataba baina ya pande hizo mbili.
Baada ya kamati ya TFF kusikiliza utetezi wa pande zote mbili, na ushahidi wa kimkataba waliamua kwamba Prince Dube alikuwa amekosea kwa mujibu wa mkataba wake na Azam FC ambao aliopaswa kuutumikia hadi mwishoni mwa Msimu huu 23/24, hivyo kama alihitaji kuondoka klabuni hapo basi alitakiwa kulipa fidia za kimkataba na waajiri wake wa zamani ndipo wamuachie,
Kabla ya sakata hili kufika TFF, Prince Dube alikuwa akihusishwa zaidi ya Yanga, Al Hilal na Simba Sc.
Yanga ina amini kwamba Prince Dube ni mrithi sahihi wa Fiston Mayele, aliyeondoka msimu uliopita na kujiunga na Pyramids FC, na tangu aondoke Mayele eneo la ushambuliaji la Yanga lilikosa kiongozi sahihi.
Simba ina amini Prince Dube atavaa vyema viatu Jean Baleke aliyekuwa kwa Mkopo klabuni hapo na kuachana nao katika dirisha dogo la usajili.
Endapo Yanga watampata Prince Dube basi watakuwa waneongeza nguvu kwenye eneo la upachikaji wa magoli, kama mchezaji huyo atakuwa sawa bila majeraha ambayo yalikuwa yakimsumbua zaidi akiwa na waajiri wake wa zamani.
Pia endapo Prince Dube atajiunga na klab ya Simba basi ataenda kuongeza idadi ya magoli klabuni hapo.
Dube yupo nchini bado na chini ya uangalizi wa mabosi wa moja klabu kubwa Tanzania hii ni baada ya kuachana dili la kujiunga na klab ya Al Hilal ya Sudan.
Dube amekuwa akiendelea na ratiba zake za kila siku za Mazoezi binafsi mara mbili kwa siku akiwa chini ya Uangalizi wa moja ya Mwalimu na Mtaalamu wa utimamu Mkubwa sana hapa Tanzania katika Moja ya Gym kubwa hapa nchini Tanzania.
Post a Comment