Djigui Diarra atikisa kiberiti Yanga SC, Kibwana ... - EDUSPORTSTZ

Latest

Djigui Diarra atikisa kiberiti Yanga SC, Kibwana ...

Djigui Diarra atikisa kiberiti Yanga SC, Kibwana ...

EURO 2024 Mechi zinaendelea leo usikose kuzitazama mechi zote za leo live bure kwenye simu yako bonyeza hapa kudownload app inarusha mechi hizi live bure kabisa pia ukiwa na app hii utaweza kutazama muvi zilizotafsiriwa pia utaweza kutazama chanel za Azam tv na dstv bure kabisa bofya sasa kudownload

Kipa wa Yanga, Djigui Diarra imedaiwa ametingisha kiberiti klabuni hapo kwa kuwataka viongozi wa kikosi hicho kumwongezea mshahara zaidi ili aendelee kusalia katika timu hiyo.

Taarifa zilizopo zinadai kipa huyo kutoka Mali, aliyejiunga na Yanga Agosti 8, 2021 akitokea Stade Malien ya nchini kwao, amewaambia mabosi wa mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho kwa misimu mitatu mfululizo thamani yake kwa sasa imepanda zaidi tofauti na mwanzo jambo linalomfanya kutaka kuboreshewa masilahi.

Kipa huyo ambaye mkataba wake alioongeza mwaka jana unafika mwishoni, amekuwa ndiye nguzo ya Yanga katika kubeba mataji kwa misimu mitatu mfululizo na kuifikisha timu hiyo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika na robo fainali ya Ligi ya Mabingwa.

UONGOZI wa Yanga uko kwenye mazungumzo na beki wa kulia wa timu hiyo, Kibwana Shomari ili kuongeza mkataba mpya. Kibwana aliyejiunga na timu hiyo Agosti 9, 2020 akitokea Mtibwa Sugar, amekuwa hana nafasi kikosi cha kwanza kutokana na uwepo wa beki mwenzake, Kouassi Yao ingawa Yanga inataka aendelee kusalia.



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz