Mfadhili wa zamani wa Simba Azim Dewji amewatuliza mashabiki wa timu hiyo kuacha kuendelea kuwashurutisha viongozi wao kujiuzulu akisema hatua hiyo itaibomoa timu yao.
Dewji ameyasema hayo leo kufuatia malumbano ya uongozi yanayoendelea ndani ya klabu hiyo.
Amewashauri viongozi wa Simba kujitokeza hadharani haraka kuwatuliza mashabiki wao huku akiwataka pia kuhakikisha wanasimamia vizuri usajili wa dirisha kubwa sambamba na kutafuta kocha ambaye atakaa kwa muda mrefu badala ya kuwa na mabadiliko ya mara kwa mara ambayo yamekuwa yakiiathiri timu hiyo.
Post a Comment