Klabu ya Azam imekamilisha usajili wa mshambuliaji Adam Adam kwa mkataba wa mwaka mmoja akiwa Mchezaji huru akitokea Mashujaa.
Taarifa ya Azam FC imeelza; "Baada ya kucheza miaka 10 nje ya viunga vya Azam Complex, hatimaye tumemrejesha kijana wetu, Adam Adam.
"Tunathibitisha kuwa tumeingia naye mkataba wa mwaka mmoja, tayari kabisa kuitumikia Azam FC msimu ujao 2023/24. Karibu sana nyumbani! Adam!"
Adam Adam amesajiliwa Azam FC baada ya msimu bora na Mashujaa aliyoifungia magoli 7.
Adam Adam amewahi kuhudumu Tanzania Prisons na amefunga magoli saba akiwa Mashujaa. Adam Adam aliwahi kucheza academy ya Azam 2011-14 hivo amerejea nyumbani.
Post a Comment