Ali Kamwe: Hakuna mchezaji atakayeondoka Yanga

Ali Kamwe: Hakuna mchezaji atakayeondoka Yanga

Ali Kamwe akiwa Wilayani Geita Mkoani Geita amewathibitishia Mashabiki na Wanachama wa Club hiyo kuwa hakuna Mchezaji yeyote atakayeondoka klabuni hapo.

Kamwe amesema malengo ya Yanga kama Club ni kwenda kuchukua vikombe vya Afrika pamoja na kuendelea kuwa tishio kwa Afrika na sio kingine.

“La msingi ambalo Rais wetu Injinia Heris amelisisitiza zaidi ya mara mbili hakuna Mchezaji bora uliyemuona msimu huu ataondoka ndani ya kikosi chetu kwenda Timu yoyote hayupo hayupo Mchezaji yoyote katika mliowaona na nyie mnasema huyu anajua ataondoka msimu huu” ——— Kamwe.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post