Ahmed Ally athibitisha Simba kuachana na Chama

Ahmed Ally athibitisha Simba kuachana na Chama

Ni yanga vs Safari champions usikose kuitazama mechi hii live bure kwenye simu yako pia mechi za EURO 2024 download app yetu inayorusha mechi hizi buree kabisa pia kwenye app yetu kuna muvi zilizo tafsiriwa kwa kiswahili pia kuna chanel za Azam tv na Dstv zote unazitazama buree download sasa App yetu kuenjoy bonyeza 👉🏻👉🏻HAPA

Ahmed Ally athibitisha Simba kuachana na Chama

Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amefunguka hatima ya mchezaji wao nyota Clatous Chota Chama ambaye anahusishwa kujiunga na watani zao, Young Africans SC.

Akizungumza na ITv katika Ofisi za Simba, kuhusu taarifa za Simba kushindwa kumbakiza Clatous Chama na kukaribia kutangazwa na wapinzani wao Klabu ya Yanga, Ahmed amesema kuwa wachezaji wanaowahitaji tayari wameshawaongezea mikataba na wameshawatangaza hivyo iwapo kuna mchezaji atasajiliwa na Yanga kutoka Simba, basi ifahamika kuwa hakuwa kwenye mipango ya Simba.

“Mchezaji yoyote ambaye atandoka Simba kwenda Yanga, fahamu ya kwamba huyo mchezaji hatakiwi Simba. Kiufupi ni kwamba hakuna timu yoyote Tanzania hii inaweza kumchukua mchezaji yoyote anayetakiwa na Simba. Ukiona mchezaji yoyote wa Simba anakwenda Yanga ujue huyo hakuwa kwenye mipango ya Simba.

“Tayari tumetangaza kuwaongezea mikataba wachezaji tunaotaka wabaki, Israel Mwenda na Muzamiru Yassini, kwa hiyo wale wote ambao tuna mipango nao, tumeshatangaza kuwaongezea mikataba mpaka 2026. Tusipomsajili ama kumuongezea mkataba mchezaji maana yake hakuwa kwenye mipango yetu,” amesema Ahmed Ally.

Wachezaji ambao mpaka wameshaongezewa mikataba na Simba ni Mzamiru Yassin, Israel Mwenda na Kibu Denis, kwa mantiki hiyo na kwa kauli ya Ahmed iwapo hawa ndiyo wachezaji pekee walioongezewa mikataba, maana yake hata Chama naye ametemwa baada ya mkataba wake kumalizika.


Hoja nzito Simba wameshindwana na Clatous Chama mezani au Simba haikimuhitaji kabisa Chama na hakukuwa na mazungumzo yoyote?

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post