Ahmed Ally ashindwa kujizuia kwa kile kinacho endelea Simba atoa tamko hili

 

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ali amewataka mashabiki wa timu hiyo kuwa watulivu wakati huu inaonekana kuwepo kwa sintofahamu

Ahmed amesema hata bahari kuna wakati huchafuka lakini baada ya machafuko kupita, utulivu hurejea

"Bahari hata ikichafuka vipi lakini kuna wakati inatulia, Wavuvi na Wasafiri wanaendelea na shughuli zao kama kawaida."

"Wavuvi na Wasafiri wenzangu msiwe na hofu punde bahari itakaa sawa na maisha yetu yataendelea kama kawaida," alisema Ahmed

Kumekuwa na sintofahamu baada ya taarifa ya kujiuzulu kwa baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi huku Wajumbe wengine kugoma kujiuzulu na kuibua kinachoonekana kama mgogoro baina ya Wajumbe wa Bodi upande wa Wanachama na Mwekezaji Mohammed Dewji

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post