Ni kama mashabiki wa Yanga walikuwa wakisubiri kwa hamu wafike Msimbazi ili waonyeshe furaha yao ya kutwaa ubingwa wa tatu mfululizo wa Ligi Kuu Bara kutokana na namna walivyokuwa wakijiachia.
Wakiwa hapo gari kubwa la Yanga lilisimama karibu kabisa na jengo la watani zao, Simba kisha kunyenyua ubingwa huo mara kadhaa huku mashabiki wao wakiitika.
Zoezi hilo lilikuwa likiongozwa na Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe huku akiwa sambamba na supastaa wa timu hiyo, Stephane Aziz KI wakitabasamu.
Wakati zoezi hilo likiendelea bendera za klabu ya Simba zilikuwa zikipepea kulia mwa msafara huo huku mashabiki wachache waliovaliaa jezi nyekundu wakishangaa kile kinachoendelea.
Huku msafara huo ukisogea taratibu ndipo ilipopiga shoti ya nyaya za umeme juu ya transform kubwa lililopo mbele ya jengo la Simba kutendo ambacho kimezua taharuki.
Shoti hiyo haikuonekana kuwa na madhara yoyote, Yanga iliendelea na ratiba zake ndipo mashabiki wachache wa Simba walipoanza kuimba jina la timu yao.
Yanga kuona hivyo ndipo wakajibu mapigo kwa kumtaja madhamini wao mkuu GSM hioja ni vingi hapa Kariakoo, watani hao wa jadi wanatambiana huku shughuli mbalimbali zikisimama kwa muda kisha msafara huo kusonga hadi makao makuu ya klabu hiyo, yaliyopo mitaa ya Twiga na Jangwani.
Post a Comment