Klabu ya Young Africans ipo kwenye mpango wa kumuongezea mkataba mpya wa mwaka mmoja kiungo wao Jonas Mkude (31) ambaye anamalizia mkataba wake ndani ya klabu hiyo.
Mkude alisajiliwa na Yanga kama mchezaji huru mwanzoni mwa msimu huu baada ya mkongwe huyo kutemwa na Simba aliyokuwa ameitumikia kwa takribani miaka 13.
Yanga walimpa Mkude mkataba wa mwaka mmoja kwa kuwa hawakuwa na uhakika kama angeweza kuwa na kiwango bora hasa ikikumbukwa kuwa hakuwa akipata nafasi ndani ya Simba kwa muda mrefu katika kipindi cha mwaka wake wa mwisho ndani ya timu hiyo.
Mkude ameonesha uwezo mkubwa katika mechi za hivi karibuni hasa zile za kimataifa (robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL) dhidi ya Mamelodi Sundowns ya nchni Afrika Kusini, jambo lililowafanya viongozi wa Yanga wafikirie kumuongezea kandarasi nyingine.
Post a Comment