Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara Yanga baada ya kukomba pointi tatu dhidi ya Mashujaa wamerejea Dar kwa maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar.
Timu hiyo imekuwa kwenye mwendo mzuri ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2023/24 kutokana na kupata matokeo chanya kwenye mechi ambazo wanacheza uwanjani.
Ipo wazi kwamba kikosi cha Yanga chini ya Miguel Gamondi baada ya kucheza mechi 25 kimekomba jumla ya pointi 65 kibindoni ni namba moja kwenye msimamo wa ligi.
Ikumbukwe kwamba katika mchezo wa mzunguko wa kwanza dhidi ya Kagera Sugar uliochezwa Uwanja wa Kaitaba, baada ya dakika 90 ubao ulisoma Kagera Sugar 0-0 Yanga.
Kiungo wa kazi Pacome Zouzoua ameanza kurejea katika ubora na mchezo dhidi ya Mashujaa alipewa dakika 20, Uwanja wa Lake Tanganyika uliposoma Mashujaa 0-1 Yanga.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex, Mei 8, 2024 kwa wababe hao kuwa kazini kusaka pointi tatu muhimu.
Ilikuwa ni Mei 5 Yanga ilikomba pointi tatu mazima mbele ya Mashujaa kwa bao la Joseph Guede dakika ya 41 akiwa ndani ya 18.
Post a Comment