Wakala na msimamizi wa kampuni ya usimamizi wa michezo ya Zambro Sports Management, Zambro Traore yupo nchini Tanzania kwaajili ya matukio mawili muhimu.
Tukio la kwanza ni kuhudhuria fainali ya kombe la shirikisho la CRDB kati ya Yanga na Azam ambapo wachezaji anaowasimamia watatu Yao Kwai, Pacome Zouzoa na Stephanie Aziz Ki watashuka dimbani na uzi wa Yanga.
Tukio lingine ni kuhusu kujadiliana na klabu ya Yanga juu ya mkatabna mpya wa Stephanie Aziz Ki baada ya mkataba wake wa awali kufikia tamati mwishoni mwa msimu huu.
Post a Comment