Tutabaki na wenye moyo wa kuitumikia Simba :- Ahmed Ally

 

Meneja wa Habari na Mwasiliano klabu ya Simba Ahmed Ali amesema tetesi nyingi za usajili kuwahusisha wachezajii wa Simba inadhihirisha ubora wa wachezaji walio katika kikosi cha Simba

Licha ya Simba kutofanya vizuri sana msimu huu, Ahmed amesema hilo haliondoi ukweli wana wachezaji wazuri

Aidha Ahmed amedokeza kuwa katika usajili wa kuelekea msimu ujao watawabakisha wachezaji wote wanaohitajika na wenye moyo wa kuitumikia Simba

"Licha ya timu yetu kusemekana ni mbovu lakini ndio timu inayoongoza kwa wachezaji wake kuhitajika na vilabu vingi zaidi vya ndani na nje nchi. Ni dhahiri kuwa tuna kikosi chenye Wachezaji bora

Hatujapata matokeo mazuri msimu huu lakini haindoi ukweli kuwa wachezaji wetu ni bora sana ndio maana wanatajwa sana sokoni

Tunachoenda kukifanya hivi sasa ni kubaki na wale bora wenye moyo wa kuitumikia Simba

Katika dirisha hili la usajili tunaemtaka atabaki Simba lengo ni kutengeneza Simba tishio turudi kwenye Ufalme wetu," aliandika Ahmed katika ukurasa wa mtandao wa kijamii

Clatous Chama na Kibu Denis ndio wachezaji wanaozungumzwa zaidi wiki hii ambapo licha ya kupewa ofa za kusaini mikataba mipya, wachezaji hao bado hawajasaini huku mikataba yao ikifika tamati mwishoni mwa mwezi huu

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post