Simba wapo tayari kumpa kila kitu Aziz KI aondoke Yanga

Simba wapo tayari kumpa kila kitu Aziz KI aondoke Yanga

Ni kesho ligi inatamatika huku ni Yanga vs Tz prison kule ni Simba vs Jkt tanzania usikose kuzitazama mechi hizi zote live buree kwenye simu yako bonyeza hapa kudownload app itakayokuwezesha kuzitazama mechi hizi live buree kabisa bofya sasa kuidownload mapema ili kuepuka usumbufu pia kwenye app hii kuna yale mambo yetu yale

Aziz KI amemaliza Mkataba wake Yanga na amegoma kusaini ofa mpya ya Yanga; wanapambana kumbakiza na Yanga hawausemi ukweli huu mchungu kwa mashabiki wao.

Menejimenti ya Simba inafanya mawasiliano na AZIZ KI; na Simba ipo tayari kutoa gharama anazotaka AZIZ KI ikiwa ni pamoja na mshahara.

Mazungumzo kati ya Simba SC Tanzania, Feitoto na Klabu yake ya Azam yanaendelea vizuri kwa makubaliano ya Simba kuona uwezekano wa kuuvunja Mkataba wake.

Aidha, Simba inaendelea kufuatilia kwa karibu sana uwezekano wa kumpata Fiston Mayele kupitia makubaliano ya mkopo kutoka Pyramids kule Egypt.

Kuhusu Moses Phiri upo uwezekano mkubwa sana wa Simba kumrejesha Kikosini kutoka Zambia; ili aungane na wenzake kwenye Pre-Season ya msimu mpya unaofuata.

Tarehe 28 Mei, 2024 kuna wachezaji wa Simba wataagwa hadharani uwanjani; siku ya mchezo wetu wa mwisho; wa kuhitimisha msimu wa mwaka huu 2023/2024.

Beki kisiki Lameck Lawi wa Coastal Union ni mali ya Simba kwa miaka miwili mfululizo. Atachukua nafasi Hamis Kazi ambaye atauzwa ama kutolewa kwa mkopo.


Henock Inonga, Esomba Onana na Saidoo Ntibazokiza wataachwa na Simba msimu ujao ili kupisha wachezaji wengine wapya wa kimataifa.

Kibu Denis Prosper ni mali ya Simba kwa miaka miwili mingine. Tayari taratibu zake za usajili mpya zimekamilika kwa asilimia zote.

Menejimenti ya Simba inafanya kila jitihada za kumbakiza Sadio Kanoute ambaye ameonyesha nia ya kutaka kuondoka Simba mwishoni mwa msimu huu.

Tutaendelea kupeana updates za taarifa za ndani kabisa kuhusu usajili wa Klabu yetu ya Simba.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post