Baadhi ya wafanya biashara wa Machinga Complex na Kariakoo, wamesimamisha shughuli zao kwa muda wakishuhudia msafara wa Yanga ukipita, huku wanaoishabikia timu hiyo wakiamsha shangwe kubwaa.
Wafanya biashara hao,wamesimama kando ya barabara, wakiangalia mashabiki na basi lililobeba wachezaji wa klabu huyo, wakipita kwa shangwe ya kusherehekea ubingwa wao wa msimu huu.
Yanga imefanya msafara huo, kutoka Uwanjani wa Benjamin Mkapa, kupitia Keko, Karume, Kariakoo ambapo kwa sasa wanaelekea Jangwani.
Mbali na wafanya biashara hao, barabara ya mwendo kasi, yanapita magari yaliopo kwenye msafara huo, Huku foleni ikiwa kubwa.
Magari ya mwendo kasi, yamelazimika kusubili kwa muda ili kuyapisha magari hayo, kwani hakukiwa na namna ya kupenya katikati ya foleni kubwa.
Kwa sasa gari lililobeba wachezaji wa Yanga,lipo Msimbazi na askari wapo imara kulinda usalama wa raia.
Lakini mashabiki wa Simba walipo Msimbazi hawajakubali unyonge, kwani wanaimba nyimbo za klabu hiyo wakipeperusha bendera juu.
Post a Comment