Shirikisho la Mpira Duniania (FIFA), lilikutana huko nchini Thailand Siku ya Jumatano, Mei, 15, 2024 katika kongamano lake la kila mwaka nakufanya tathmini ya kiwango gani mechi za michuano ya ndani zilizochezwa kwenye mabara mengine au nje ya nchi ambazo siyo asili zimefanikiwa.
(Mfano mechi ya El clasicco kuchezwa USA na zinginezo ni kwa kiwango gani zimefanikiwa na matokeo au mapokeo yake yamekuwaje)
FIFA ilitangaza kwamba wanachama 10 hadi 15 wanaowakilisha vyama vya kitaifa, mashirikisho, vilabu, ligi, wachezaji, vikundi vya mashabiki na mashirika binafsi watakutana tena ili kutoa mapendekezo juu ya suala hilo katika miezi ifuatayo.
Iwapo wakijiridhisha na kuona utaratibu huo ni mzuri na unafaa FIFA watatoa fursa kwa baadhi ya mechi zingine za ligi ambazo zinamsisimko mbele ya mashabiki kuchezwa kwenye nchi au bara lingine.
Post a Comment