Baada ya mchezo kumalizika kiungo mshambuliaji wa Yanga ambaye ni Mfungaji bora kwa msimu huu (2023/24 ) Stephane Aziz Ki , kwenye mazungumzo na kituo cha habari cha Azamtvsports amejipongeza kwa msimu mzuri lakini ametoa kauli inayoashiria kuwa msimu ujao ataendelea kubaki Yanga , Aziz amesema
“Nitakuwa bora zaidi msimu ujao nikiwa na timu hii hii inshaAllah”
Kauli hiyo inazidi kuacha maswali kwa Mashabiki kwani inasemekana amemaliza Mkataba wake ndani ya Yanga na hajamalizan na uongozi kusaini Mkataba mpya.
Tayari inasemekana kuna vilabu kadhaa kutoka Barani Afrika vimeonesha nia ya kumuhitaji Staa huyo.
Post a Comment