Klabu ya soka ya Azam imefikia makubaliano na Klabu ya Stade Malien (Mali) kumsajili kiungo mshambuliaji, Franck Tiesse kwa mkataba wa miaka miwili kuanzia msimu ujao wa 2024-25.
Tiesse (26) anayesifika kwa uwezo wake mkubwa wa kushambulia kwa kasi na uwezo wa kutumia miguu yote miwili, akiwa Stade Malien aliisaidia klabu hiyo kufika robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu.
Nyota huyo raia wa Mali anamudu kucheza kama winga wa kulia, kiungo mshambuliaji na winga wa kushoto.
Kabla ya kumsainisha kandarasi hiyo, Azam wamemfanyia vipimo mchezaji huyo katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam ili kujua hali ya afya yake kabla ya kuanza kuwatumikia wauza Ukwaju hao wa Dar.
"Tumefikia makubaliano na klabu ya Stade Malien (Mali) ya kumsajili kiungo mshambuliaji wao, Franck Tiesse.
"Nyota huyo Muivory Coast, amekubali kusaini mkataba wa miaka miwili utakaonza rasmi msimu ujao 2024/25. Welcome to Azam FC, Tiesse!." Imesema taarifa ya Azam FC.
Post a Comment