Taarifa kutoka chanzo chetu ndani ya Klabu ya Simba zinaeleza kuwa kuna kila dalili ya Simba kumpoteza kipa wao namba moja wa sasa, raia wa Morocco Ayoub Lakred.
Uongozi wa Simba bado hauna uhakika wa kusalia kwa kipa wao namba moja Ayoub Lakred ambaye inaelezwa huenda akaachana na timu hiyo baada ya kumaliza mkataba wake mwisho wa msimu huu.
Ayoub alijiunga na Yanga mwanzoni mwa msimu huu akitokea FAR Rabat ya nyumbani kwao Morocco, lakini miamba ya soka ya Morocco, Wydad Casablanca inadaiwa kuwa wameonesha nia ya kumtaka kipa huyo mwenye umri wa miaka 28.
Post a Comment