Al Ahly, Pyramids, Mamelodi wapigana vikumbo kumng'oa Aziz Ki Yanga

Aziz Ki na Kocha wa Mamelodi

Ni leo Simba vs Geita gold usikose kuitazama mechi hii live buree kupitia simu yako bonyeza hapa kudownload app itakayorusha mechi hii live bureee kabisa bofya sasa

Taarifa za kuaminika ni kuwa Klabu za Espérance de Tunis na Pyramids zipo kwenye mazungumzo rasmi na wakala wa kiungo mshambuliaji wa klabu ya Yanga, Stephane KI Aziz ili kupata saini yake kuelekea msimu ujao.

Inaelezwa kuwa, vigogo hao kila mmoja wao inapambana kwa wakati wake ili kupata huduma ya mchezaji huyo.

Stephane KI Aziz bado hajasaini karatasi zozote mpaka sasa katika Klabu ya Yanga kwa mkataba mpya, huku klabu za Al Masry, MC Alger na Al Ahly zimetoa ofa thabiti kwenye menejimenti ya mchezaji huyo wa zamani wa ASEC Mimosas.

Wengine ni Mamelodi Sundowns na Kaizer Chief zimejiweka pembeni kwenye kinyang'anyiro cha kuwania saini ya KI Aziz.

Kwa upande wa mabingwa wa kihistoria wa Tanzania, Yanga bado wanaendelea na harakati za kumuongezea mkataba mpya mchezaji wao.


Klabu ya Yanga kupitia kwa Ofisa Habari wao, Ally Kamwe amekiri kuwa vipo vilabu vingi nje ya Tanzania ambavyo vimeonesha nia ya kumtaka mchezaji huyo ambaye anapngoza kwa mabao kwenye ligi kuu mpaka sasa.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post