Kiungo Mkabaji wa Singida Fountain Gate Yusuph Kagoma amefikia Maamuzi ya kujiondoa ndani ya kambi ya klabu yake hiyo kufuatia kutolipwa mshahara wake wa miezi mitatu (3) mfululizo ndani ya kikosi hicho.
Kwa sasa kiungo huyo yupo nyumbani kwao Kigoma akisubiria kulipwa stahiki zake ndipo arejee katika kikosi hicho.
Mkataba wa Yusuph Kagoma na klabu ya Singida Fountain Gate unaisha mwishoni mwa msimu huu na taarifa zilizopo ni kuwa hana mpango wa kuongeza mkataba.
Inasemekana mchezaji huyo yuko katika hatua nzuri kusaini mkataba mpya na klabu ya Yanga ili akawe mbadala wa kiungo Zawadi Mauya.
Post a Comment