Klabu ya Yanga SC imeanza kuhusishwa na kuhitaji huduma ya straika Makabi Lilepo raia wa kongo msimu ujao, Yanga SC wanafanya kila mbinu wampate msimu ujao iwe kwa mkopo au kumnunua kwa jumla hasa baada ya timu yake kushuka daraja huko nchini Ufaransa.
makabi Lilepo alifanya vyema msimu uliopita akiwa na Al-Hilal katika Ligi ya Mabingwa Afrika, akifunga mabao 5 na kushiriki katika mashindano mbalimbali akiwa na klabu yake ya Al hilal ya Sudan.
Kutokana na malengo makubwa waliyonayo kuelekea Msimu Ujao kuanzia ligi ya ndani na Kimataifa, Uongozi wa Klabu ya Yanga knataka kuimarisha timu yao hasa katika eneo la ushambuliaji.
Klabu yake ya sasa ya nchini Ufaransa imeshuka daraka na hii inaweza kuwa rahisi kwa Young Africans kumpata na malengo yao kumnunua moja kwa moja na ikishindikana basi wamchukue kwa mkopo.
Post a Comment