Siku za hivi karibuni Wakala Zambro Traore aliwasili Nchini Tanzania ili kuja kujadili Kandarasi za Wachezaji wake Ususani Stephen Azizi KI ambaye kandarasi yake Inaishia Mwezi Juni Mwaka huu 2024.
Zambro Traore aliyehusika kwenye Mchakato wa Kumuuza Fiston Kalala Mayele Kwenda Pyramids kwa dau nono Amekuwa na Mahusiano mazuri na Klabu ya Yanga kwani anawachezaji 4 katika Klabu ya Yanga.
Stephen Azizi KI
Pacome Zouazoa
Yao Koussi
Joseph Guede
Kwa taarifa zilizonifikia Stephen Azizi Ki kashasaini Kandarasi Nyengine ya Kuweza Kumbakiza Yanga kwa Msimu Miwili 2024/27.
“Ndiyo, Mkataba wake (Aziz Ki) utamalizika Juni. Baada ya hapo atakuwa huru - Mchezaji huru, na muda huu ninavyoongea na wewe, Nipo Tanzania kwa sababu klabu (Yanga) imeniruhusu nije kufanya majadiliano”
“Wanataka kumuongezea Mkataba. Wametupa na ofa, ambayo wamenitumia ili kuongeza mkataba wake” Zambro Traore.
Post a Comment