Kuelekea kwenye mchezo wa kesho JKT Tanzania dhidi ya Yanga Africas, Kocha mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema hawawezi kuzungumzia sana maandalizi kwa sababu Jumamosi wametoka kucheza mechi.
Kuhusu majeraha kwa wachezaji wake Gamondi amesema wachezaji wote wapo vizuri isipokuwa kwa Joyce Lomalisa ambaye aliumia juzi na jana jioni alianza kufanya mazoezi mepesi lakini kwa upande wa Pacome Zouzoua bado hayupo tayari kucheza mchezo huo wa kesho.
“Wachezaji wote wako tayari kwa mchezo kasoro Lomalisa ambaye aliumia kwenye mchezo wa juzi dhidi ya Simba lakini jana ameanza mazoezi mepesi. Pacome yeye bado hayuko tayari kucheza kwa sababu bado yupo kwenye uangalizi wa madaktari huenda wiki hii akaanza kufanya mazoezi ya utimamu ‘fitness’.
“Ishu yake ilikuwa ni takribani mwezi mzima, hajafanya mazoezi na itachukua muda kidogo kuingia kwenye kikosi lakini kwa kesho haiwezekani lakini tutaona maendeleo yake,” amesema Gamondi.
Gamondi amesema mechi dhidi ya JKT itakuwa ya ushindani mkubwa kwa sababu utakuwa mchezo mwingine na anaimani wapinzani wake watakuja kivingine tofauti na walipokutana mechi ya mzunguko wa kwanza.
Post a Comment