Beki wa kati wa klabu ya Simba, Henock Inonga ameuambia Uongozi wa Simba kuwa anahitaji kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu na klabu imempa taarifa kuwa wameshakubali matakwa yake na atapewa baraka zote akiondoka rasmi.
Taarifa za kuaminika ni kuwa klabu ya Simba ilikuwa ikisubiri mrejesho kutoka kwa Abdelhak Benchikha ili klabu imshawishi abaki au wamuachie andoke klabuni hapo, FAR Rabat kutoka Morocco inatajwa kumalizana nae kwa mkataba wa awali na Henock Inonga.
Simba inajiandaa na maisha bila na beki wao wa kimataifa wa DR Congo, Henock Inonga kuelekea msimu ujao.
Post a Comment