Ahmed Ally akubali yaishe "Simba inapitia wakati mgumu ila wanaongeza chumvi "

Ahmed Ally.

Kesho ni Simba vs Ihefu usikose kuitazama mechi hii live ( mubashara ) kupitia simu yako bonyeza hapa kudownload app yetu buree kabisa ili usipitwe na mechi hii

Kutoka kwa Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally;

“Timu yetu inapitia kipindi kigumu Lakini ni tofauti na inavyozungumzwa yaani wanaongeza chumvi huu ni mpango wa makusudi unaoratibiwa na wasiotutakia mema, Bahati mbaya ni kwamba WanaSimba tumeingia kwenye mtego wa kujidharau na kujitukana.

“Tukiwa na Simba Bora sana tuliwahi kutolewa hatua ya awali ya ligi ya Mabingwa Afrika na UD Songo, Tukiwa na Simba Bora tuliwahi kutolewa na Green Warrios kwenye Kombe la Shirikisho Haya ni Maisha ya kawaida kwenye mpira wa miguu kila timu ya mpira hupitia nyakati kama hizi, lla tukipitia Simba basi huonekana ni kitu cha ajabu inawezekana tunahukumiwa na ukubwa wetu.

“Leo watakuambia wachezaji wabovu, kesho Muwekezaji tatizo, kesho kutwa Viongozi hawafai Hivi tungekua na matatizo yote hayo si tungekua tumeshuka daraja?

“Wengine wanaibuka kukashifu viongozi na kudhihaki wachezaji wakiamini huko ndio kuipenda Simba au wao ndio wenye uchungu sana na Simba, wakati Nyuma Mwiko wako dhofli hali waliibuka na kauli ya kusema tumeipenda wenyewe acha itue, Hii ilikuwa kauli ya kishujaa sana na waliamua kufa na timu yao.

"Kwa sasa hatuna budi kusimama na timu yetu ili mambo yasiharibike zaidi, hatuwezi kubadili yaliyopita ila tunawezakutengeneza yajayo.


“Tulichobakiwa nacho ni Ligi Kuu ya NBC, Kwa pamoja tuwekeze nguvu kwenye kombe hili, Pengo ni alama 4 tukisimama sawa sawa kwa umoja wetu tunaliondoa.

“Hii inaanza na mechi ya Tarehe 13 dhidi ya lhefu, na baada ya hapo mechi ya tarehe 20, tukichukua alama 6 kwenye mechi hizi tutakua pazuri sana Lets go Wanasimba,” Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba Sc, Ahmed Ally.

JIUNGE NA GROUP LA WAKUBA HAPA 18+ HAPA


PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE  HAPA

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post