Simba imeitwa 'Makolo' sababu ya Mo, wachezaji hawajalipwa - Luambano

Simba imeitwa 'Makolo' sababu ya Mo, wachezaji hawajalipwa - Luambano

Ni leo Dodoma Jiji vs Yanga usikose kuitazama mechi hii Live bureee kupitia simu yako bonyeza hapa kudownload app inayirusha mechi hii bure kabisa

Mtangazaji wa michezo wa kituo cha radio cha Clouds FM, Alex Luambano amesema kuwa tatizo lililopo Simba SC kwa sasa ni mwekezaji wao Mohammed Dewji 'Mo' kwani ameshindwa kutoa pesa kwa ajili ya usajili na uendeshaji wa mambo mbalimbali ya timu na na kuitelekeza timu kwa wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa klabu hiyo.

Luambano amesema hiyo ndiyo sababu kubwa ya Simba SC kuyymba na kupata matokeo mabovu ikiwemo kuishia robo fainali ya CAFCL, na robo fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB Bank.

"Hii Simba leo inaitwa 'Makolo' (jina la utani) ni kwa sababu ya Mo, jezi imejaa makolokolo (matangazo ya bidhaa za Mo) jina la makolo limetokana na bidhaa za Mo.

"Nimefanya tafiti, kuna wachezaji wanadai signing fee (ada ya uhamisho/usajili), bonus zinalipwa on time kwa sababu wanaoahidi ni Try Again na Mangungu na wanaahidi za ndani ya uwezo wao.


"Yeye sasa hivi kakaa mbali ,ikitokea lawama ni Mangungu na Try Again lakini anayewafanya Simba wamefika hapa ni Mo," amesema Luambano.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post