Sababu ya Chama kwenda Yanga ni hii

Sababu ya Chama kwenda Yanga ni hii

Kudadeki ni Namungo vs Simba ligi kuu tz bara unaanzaje kukosa kuitazama mechi hii live buree kabisa bonyeza hapa kudownload app itakayorusha mechi hii live buree bofya sasa

Taarifa ambazo hazijadhibitishwa zinasema kuwa kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba, Clatus Chama huenda msimu ujao akaibukia katika mitaa ya twiga na Jangwani ambapo ameandaliwa mkataba mnono.

Chama ameshaamua kuondoka katika klabu yake hiyo baada ya kutokuwa na furaha Kwa siku za karibuni hapa ambapo amepitia misukosuko kadhaa ikiwemo kutuhimiwa kuihujumu klabu hiyo pamoja na kupewa makosa ya kinidhamu ambayo uongozi ulishindwa kuthibishisha ingawa walisema hadharani na kumsimamisha mchezaji huyo.

Ikumbukwe kuwa Chama amecheza katika klabu hiyo kwa kiwango kikubwa tangu amejiunga na kufikia hatua ya kuibeba timu hiyo mabegani mwake Kwa kuivusha mara kadhaa katika hatua za juu za michuano ya vilabu barani Afrika akifunga magoli yasiyowezekana.

Mchezaji huyo anaamua kuondoka baada ya kuona hapewi thamani anayostahili katika klabu hiyo aliyoifanyia mambo makubwa tofauti na wachezaji wengine huku mkataba wake ukifikia ukingoni mwishoni mwa msimu huu.

Mwanzoni mwa msimu huu Chama aligoma kujiunga na Kambi ya timu hiyo nchini Uturuki akishinikiza kulipwa stahiki zake na kuingia kwenye mgogoro na viongozi wake mpaka alipolipwa ndipo alijiunga na Kambi ya timu hiyo.


Taarifa kutoka Kwa rafiki wa mchezaji huyo zinasema kuwa kiungo mshambuliaji huyo ameshaamua kuondoka katika klabu hiyo na msimu ujao kuna asilimia kubwa akacheza Yanga japo Azam FC pia imempa ofa.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post