Rais Samia Suluhu Hassan amesema amefurahishwa na matukio mbalimbali yaliyoandaliwa katika shamra shamra za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Akizungumza katika Sherehe za Maadhimisho hayo leo Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam Rais amesema amefurahishwa na kurejeshwa tena kwa Ligi ya Muungano.
"Ninawashukuru waandaji wa mashindano mbalimbali yakiwemo ya mpira wa miguu ya Muungano ambayo timu ya mdogo angu Kassim imeingia Fainali lakini wasiwadharau sana Azam huenda matokeo yakawa mengine kabisa" amesema Rais Samia.
Ikumbukwe Simba na Azam FC zitacheza mchezo wa Fainali ya michuano hiyo Aprili 27, 2024 ikiwa imepita miaka 20 bila uwepo michuano hiyo.
Post a Comment