Polisi nchini Rwanda wameanza uchunguzi wa kifo cha ghafla kocha wa viungo wa klabu ya APR Adel Zrane raia wa Tunisia.
Kocha huyo amefariki Dunia akiwa nyumbani kwake jana mchana ambapo kwamujibu wa taarifa zilizotolewa na klabu yake ni kuwa hakuwa na dalili zozote za kuumwa na mchana wa leo alipaswa kushiriki ratiba ya mazoezi na timu hiyo.
Kwa mujibu wa mahojiano aliyofanya mwandishi wa habari za michezo @mickyjnrofficial na mmoja wa viongozi wa APR ni kuwa dereva wake alimpitia nyumbani kwake kwaajili ya kumchukua kwenda mazoezini kama kawaida.
Lakini alipofika na kujaribu kuita hakuitikiwa na simu yake haikupokelewa ndipo alipowajulisha viongozi ambao baada ya kufika waliamua kuvunja mlango wa nyumbani kwake na kuingia ndani ambapo walikuta kocha huyo akiwa amefariki Dunia kitandani kwake.
Kwenye salamu zake za rambirambi kiungo wa zamani wa Simba SC Thadeo Lwanga alifichua kuwa aliwasiliana kwa njia ya simu na kocha huyo usiku wa kuamkia leo na alikuwa mzima wa afya
Adel Zrane amewahi kuitumikia kwa mafanikio makubwa Simba SC chini ya makocha mbalimbali akiwemo Patrick Aussem.
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPA
Post a Comment