Afisa Habari wa Yanga SC, Ali Kamwe, amesema hakuna mchezaji yeyote mwenye mawazo ya kundoka Yanga.
Amesema kitendo cha wachezaji wao kutakiwa na timu mbalimbali kinatakiwa kuchukuliwa kwa mawazo chanya maana kinadhihirisha wana timu nzuri lakini hata hivyo wachezaji hao hawawezi kuondoka maana Yanga ndio mahali sahihi.
"Wewe ndio Mzize nyuma yako kuna Max, Aucho, Mudathir utaondoka uende wapi? Ukacheze na nani?," alisema Kamwe.
Hivi karibuni kumeibuka tetesi kuwa Simba SC wanamtaka beki wa Yanga, Bakari Mwamnyeto lakini pia, Azam FC wamepeleka rasmi ofa ya kumtaka mshambuliaji Clement Mzize.
Post a Comment