Mshambuliaji wa Pyramids FC ya Misri, Fiston Kalala Mayele amefanya mahojiano ya Simba TV kuelekea mchezo wa robo fainali ya CAFCL kati ya Al Ahly na Simba SC utakaopigwa leo nchini humo.
Akihojiwa na Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, Mayele ambaye amewahi kukipiga katika Klabu ya Yanga amesema kuwa Simba wanayo nafasi ya kufanya vizuri endapo watarekebisha mambo machache.
Ahmed: Wewe unaijua vizuri Ally Ahly, ubora wao na udhaifu wao upo wapi?
Mayele: Ni kweli kwa sababu tunacheza ligi moja, lakini Al Ahly ya msimu huu imeshuka kiwango tofauti na misimu iliyopita. Hawajafanya usajili sana wanatumia wachezaji walewale miaka yote, wachezaji nao wanachoka kwa sababu mechi ni nyingi na mashindano ni mengi.
Ahly wakiingia hatua kama hii (robo fainali) wanabadilika. Hapa Misri mechi kuahirishwa ni ngumu lakini wao wamepambana mpaka wameruhusiwa kusogezewa mbele mechi zao ili wajiandae vizuri kucheza na nyinyi, kwa hiyo wamejiandaa kwelikweli.
Ahmed: Simba wafanye nini kupata ushindi?
Mayele: Hapo ni kutembea mtu na mtu, kila anapokanyaga upo mpaka waseme leo kazi tunayo. Mechi kama hii inahitaji watu wenye uwezo wa kuamua mechi wenyewe, Simba wanaye Chama.
Aidha, Mayele amesema kuwa kuhusu kutua Simba, lolote linaweza kutokea msimu ujao.
Ahmed: Wanasimba wanakusubiri kwa hamu
Mayele: Tumuombe Munguvtumalize msimu salama, InshaAllah chochote kinawezekana.
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPA
Post a Comment