Mshambuliaji wa Pyramids FC ya nchini Misri, Fiston Kalala Mayele amewapa nafasi waajiri wake wa zamani, Klabu ya Yanga kuifunga Mamelodi Sundowns na kutinga hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mayele ambaye amewahi kuitumikia Yanga kwa mafanikio makubwa ndani ya miaka miwili kabla ya kutimkia Misri, amesema kuwa Yanga wanayo nafasi kubwa ya kutoboa mbele ya Mamelodi, hivyo wanapaswa kujituma na kucheza kwa nidhamu ili kufikia malengo waliojiwekea.
Itakumbukwa kuwa, Pyramids walikuwa kundi moja na Mamelodi ambapo katika mchezo wa kwanza nchini Afrika Kusini walitoa sare lakini wakapoteza kwa bao moja wakiwa nyumbani kwao Misri kwenye mchezo wa pili.
"Mamelodi wananikera sana wanavyocheza pasipasi nyingi, mimi nawapa Yanga nafasi kubwa kushinda kama Simba, wametoa droo nyumbani wanaenda kuimaliza mechi ugenini, sisi Pyramids FC tulitoa nao droo nyumbani kwao Afrika Kusini, nawapa Yanga ushindi kesho (leo).
"Simba kama watakuwa makini kesho (leo) watashinda kwa Al Ahly, nimeiona mechi ya kwanza Simba walicheza vizuri sana, nakumbuka baada ya mechi niliwapigia simu Inonga na Fabrice Ngoma nikawaambia msikate tamaa mmecheza vizuri mnaweza kushinda nyumbani kwao," amesema Mayele.
Yanga watakuwa na kibarua kigumu leo mbele ya Mamelodi katika dimba la Loftus Versfeld huko Pretoria nchini Afrika Kusini baada ya mchezo wa kwanza kumalizka kwa suluhu katika dimba la Mkapa weekend iliyopita.
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPA
Post a Comment