Shabiki kindakindaki wa Klabu ya Simba maarufu kwa jina la GB 64 amesema kuwa viongozi wa timu hiyo wamemwachia Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu, Ahemd Ally huku wao wakiendelea na mambo yao binafsi baada ya kuona inafanya vibaya.
GB 64 amesema kuwa si Mwenyekiti wa Klabu, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa CEO wa Klabu ambaye kwa sasa yupo karibu na timu badala yake wamemwachia Ahmed afanye kila kitu jambo ambalo linaifanya timu isipate matokeo chanya uwanjani.
GB 64 ameongeza kuwa iwapo watafungwa na watani zao Yanga kwenye mchezo wa dabi Aprili 20, kwenye Dimba la Mkapa basi watawawajibisha viongozi wao palepale uwanjani.
“Tukifungwa kwenye dabi labda wasije uwanjani pale. Mashabiki tusiisuse timu yetu twende tukaishabikie, mbivu na mbichi zitajulikana kwa Mkapa, Aprili 20. Tukipigwa bao 5 palepale hatoki mtu.
“Ile mechi ya Kigoma (dhidi ya Mashujaa FC), viongozi na mashabiki hawakwenda, lakini Aprili 20 twendeni tukaujaze uwanja tuisapoti timu yetu. Kimetokea cha kutokea hata tukifungwa goli moja pale hatoki kiongozi.
“Hizo ndizo salam tunawapa, basi kama ni chawa au mamluki itajulikana pale,” amesema GB 64.
Simba kwa sasa inapitia wakati mgumu huku hivi karibuni ikiondoshwa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kuondoshwa pia kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Tanzania na inashika nafasi ya tatu kwenye Ligi baada ya kutoa sare jana na Singida Black Stars (zamani Ihefu FC).
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPA
Post a Comment