Kiungo mshambuliaji wa Simba, Kibu Denis anamaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu 2023/24 na viongozi wa Simba tayari wameshazungumza kuhusu ofa nyingine, mchezaji yupo tayari kuendelea kusalia Simba.
Clatous Chama chaguo lake la kwanza ni kubaki Simba, ameshaweka ofa yake mezani anahitaji miaka miwili na kiasi anachotaka, Uongozi umeshapeleka ofa ya Chama kwa Muwekezaji.
Israel Mwenda anatazamiwa kama mbadala sahihi kwa Shomari Kapombe, yupo kwenye mpango wa Simba msimu ujao, viongozi wanaamini msimu ujao utakuwa ndio muda sahihi kwake kutumika ofa yake wanayo na wamekubali kubaki nae msimu ujao.
Ayoub Lakred ambae inaelezwa kulikuwa na ofa ya Wydad Casablanca, lakini viongozi wanapambana kuhakikisha anaendelea kusalia Simba kwa misimu mingine zaidi baada ya sasa kusaini mwaka mmoja, amewaeleza viongozi wa Simba wameichukua wapo nayo mezani na ikiwezekana ataendelea kusalia Simba msimu ujao.
Taarifa za Kibu Denis, Israel Mwenda, Clatous Chama na Ayoub Lakred za kumaliza kandarasi zao mwishoni mwa msimu wa 2023/24 zipo mezani kwa muwekezaji miezi sita sasa.
Post a Comment