Jobe, Fred kupewa 'Thank you' na Simba

Jobe, Fred kupewa 'Thank you' na Simba

Tayari Joto la Dabi ya kariakoo limeanza hivi unaanzaje kukosa kuitazama mechi hii bonyeza hapa kudownload app itakayorusha mechi hii live bureee kupitia simu yako bonyeza sasa kuipakua mapema ili kuepuka usumbufu siku ya mechi

Washambuliaji wa Simba Sc, Pa Omar Jobe na Freddy Koubalan huenda huu ndiyo ukawa msimu wao wa kwanza na wa mwisho kuonekana katika Ligi Kuu Tanzania Bara kutokana na moja ya mashart ya mkabata wao waliosaini na klabu ya Simba ni kuonyesha kiwango bora na cha kuisaidia timu kwa nyakati zote.

Kwa mujibu wa chanzo chetu ambacho hakikupenda kutwaja jina; kimesema wachezaji hao walipewa mkabata wa miezi sita wenye kipengele cha iwapo wakifanya vizuri wataongezewa mkabata.

Nyota hao waliosajiliwa kwa pamoja kwenye dirisha dogo la msimu uliopita wakichukua nafasi ya Moses Phiri na Jean Othos Baleke, wameshindwa kuonesha ubora na kuisaidia timu hiyo pakubwa kama ambavyo yalikuwa matarajio ya Wanamsimbazi.

Tayari maneno ni mengi kutoka kwa mashabiki na wanachama wa Simba na hata viongozi wa zamani na wa sasa wa Simba wakiponda usajili wa wachezaji hao kuwa hauna tija wala haujawa na matunda kwenye kuchagiza malengo na mafanikio ya klabu.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post