Kikosi cha wachezaji 25 wa Yanga SC na viongozi wa Benchi la Ufundi wakiongozwa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi, kinatarajiwa kusafiri leo saa 2 usiku kuelekea jijini Mwanza kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Singida Fountain Gate.
Mchezo huo ambao utakuwa wa 21 kwa timu yetu ndani ya ligi hiyo, unatarajiwa kuchezwa kesho Jumapili saa 10 jioni kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
“Baada ya kumalizana na Dodoma Jiji, kikosi chetu kitaondoka leo (jana) saa 2:00 usiku kuelekea Mwanza kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Singida Fountain Gate FC. Uzuri wa ni kwamba Mwanza ni ngome ya Yanga.
“Tunaamini mchezo utakuwa mzuri na wenye ushindani lakini tunaamini kwenye ubora wa wachezaji wetu, maandalizi na mipango yetu itatupa matokeo mazuri," amesema Ally kamwe, Ofisa Habari wa Yanga.
Wachezaji watakaoondoka ni; Djigui Diarra, Aboutwalib Mshery, Ibrahim Bacca, Dickson Job, Nickson Kibabage, Lomalisa Mutambala, Zawadi Mauya, Gift Fred, Maxi Nzengeli, Skudu Makudubela, Jonas Mkude na Farid Mussa.
Wengine ni; Clement Mzize, Mudathir Yahya, Khalid Aucho, Augustine Okrah, Joseph Guede, Stephane Aziz Ki, Kibwana Shomari, Denis Nkane, Sheikhan Khamis, Salum Abubakar, Pacome Zouzoua, Yao Attohoula na Kennedy Musonda.
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPA
Post a Comment