Droo ya Robo Fainali ya CRDB Confederation Cup imechezwa mchana huu na timu nane zimeshawajua wapinzani wao.
Azam FC itakipiga dhidi ya Namungo FC, Yanga SC dhidi ya Tabora United, Coastal Union itavaana na Geita Gold na Ihefu SC itamenyana na Mashujaa.
Nusu Fainali, mshindi kati ya Azam na Namungo atacheza na mshindi kati ya Coastal Union na Geita huku mshindi kati ya Ihefu na Mashujaa, atakipiga na mshindi kati ya Yanga na Tabora.
Post a Comment