Klabu ya Yanga SC, imefungiwa kufanya usajili na FIFA kwa kukiuka kanuni za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu FIFA.
Uamuzi huo umefanywa na FIFA baada ya klabu hiyo kukiuka Annee 3 ya kanuni ya uhamisho wa wachezaji RSTP ya Shirikisho hilo.
Pamoja na masuala mengine, Yanga haikuingiza uthibitisho wa malipo ya uhamisho ya mchezaji husika katika Mfumo wa Usajili TMS licha ya kukumbushwa kufanya hivyo.
Klabu hiyo imetakiwa kutekeleza matakwa hayo ya kikanuni na kuwasilisha taarifa ya Kamati ya Nidhamu ya FIFA ambapo suala hilo limefikishwa kwa ajili ya hatua zaidi.
Kutokana na uamuzi huo wa FIFA, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzaia TFF limeifungia kufanya usajili kwa wachezaji wa ndani.
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPA
Post a Comment