Baada ya kutupia bao lake la 14 kwenye ligi kuu na kuongoza kwenye chati ya upachikaji mabao akimuacha Feisal Salum 'Fei Toto' (13), ameapa kuifunga Simba Jumamosi.
Yanga watakaokuwa wenyeji wa Simba Jumamosi watashuka kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam wakiwa na kumbukumbu ya kumfunga mtani wao kwa mabao 5-1.
Kupitia mtandao wa kijamii wa 'Instagram' wa Waziri wa Madini, Anthony Mavunde ambaye alimpongeza Aziz KI kwa kutupia bao la 14 katika mchezo dhidi ya Singida Fountain Gate jana, Yanga wakiibuka na ushindi wa mabao 3-0, amemuahidi kumpa zawadi ya bao Jumamosi dhidi ya Simba.
"Asante boss naamini nitafanya zaidi mbeleni na kwenye mchezo ujao bao n'takalofunga litakuwa maalumu kwa ajili yako," ameandika Azik KI akijibu pongezi kutoka kwa kiongozi huyo.
Na mchezo ulio mbele ya Yanga ni dhidi ya Simba na tayari kiungo huyo ameifunga Simba mara mbili kwenye mechi ya msimu uliopita iliyochezwa Oktoba 23, 2022 matokeo yakiwa bao 1-1.
Katika mchezo huo mabao yalifungwa na Aziz KI kwa mpira wa kutengwa katika dakika 45 za kipindi cha kwanza, huku bao kwa upande wa Simba likifungwa na Augustine Okrah dakika ya 14.
Bao la pili Aziz KI kuifunga Simba ni msimu huu mzunguko wa kwanza ambapo alifunga lile la tatu katika kichapo cha mabao 5-1 huku mengine yakifungwa na Maxi Nzengeli aliyefunga mawili, Pacome Zouzoua kwa mkwaju wa penalti na Kennedy Musonda.
Post a Comment