Yanga wanaweza kuandika histori Mpya hapa

Yanga ina nafasi ya kuandika historia

Kivumbi Leo Usikose kuitazama mechi ya Al ahly vs Yanga live bure kupitia simu yako download app yetu itakayokuwezesha kuitazam mechi live bure bonyeza hapa Sasa kuidownload

Mwaka jana, Yanga ilishtua Afrika baada ya kutinga hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika ingawa kwa bahati mbaya ikalikosa kombe hilo mbele ya USM Alger ya Algeria.

Unaweza kusema ililikosa kwa bahati mbaya tu maana mechi mbili baina yao zilimalizika kwa sare ya mabao 2-2 lakini Waalgeria walichukua ubingwa kwa vile walipata idadi kubwa ya mabao ugenini hapa Dar es Salaam ambapo walishinda mabao 2-1 na wakachapwa bao 1-0 kwao.

Tunaweza kusema ilishtua kwa vile haikuwa na mwanzo mzuri kwenye hatua ya makundi ya mashindano hayo kwani ilifungwa mabao 2-0 na Monastir ya Tunisia katika mechi ya kwanza ambayo ilicheza ugenini.

Msimu huu ikafanikiwa kuingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kutofanya hivyo kwa muda mrefu na ikaanza vibaya kama ilivyokuwa msimu uliopita ambapo ilifungwa mabao 3-0 na CR Belouizdad ugenini huko Algeria katika mechi ya kwanza.

Hata hivyo, ikapindua meza kibabe na sasa ni miongoni mwa timu sita ambazo zimetangulia mapema katika hatua ya robo fainali nyingine zikiwa ni Al Ahly, Mamelodi Sundowns, TP Mazembe, Petro Luanda na Asec Mimosas.

Yanga haijafika hatua hiyo ya robo fainali kwa kubahatisha kwani imeonyesha kiwango bora kwenye mechi za mwishoni za hatua ya makundi hasa mechi ya mwisho dhidi ya CR Belouizdad ambayo ilishinda mabao 4-0.

Inaonyesha ubora wa kitimu kwa kufanyia vyema kazi mbinu za kocha Miguel Gamondi lakini pia wachezaji mmoja mmoja wamekuwa wakicheza kwa kujituma kwa dakika zote za mchezo kuhakikisha timu yao inapata matokeo mazuri.


Nje ya uwanja, imekuwa ikipata sapoti kubwa ya mashabiki ambao muda wote wamekuwa wakiwashangilia wachezaji jambo ambalo linawaongezea ari ya kupambana na kuzipa ugumu timu pinzani ambazo zinakutana nayo.

Uongozi nao umekuwa ukihakikisha timu inakuwa katika hali ya utulivu na inapata mahitaji stahiki kabla na baada ya mechi zao na hivyo kuwa chachu ya kupata matokeo mazuri katika mechi zao.

Kwa namna inavyoenda, kama itazidisha hiki ambacho inakifanya inaweza kutoboa tena kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu kwa kufika mbali.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post