Klabu ya Yanga wanahitaji sana duma ya mshambuliaji wa Azam FC, Prince Dube. Wanaamini Dube anaweza kuwa mtu sahihi wa kuziba nafasi ya Fiston Mayele.
Inaaminika kwamba Yanga wamekuwa wakihangaika kumshawishi mchezaji huyo kwa muda mrefu kutua katika kikosi hicho kutokana na uwezo wake.
Hivi karibuni wakati Azam FC ikiwa mikoani kwa mechi za Ligi Kuu, Dube alionekana kwenye Uwanja wa Mkapa akishuhudia mechi ya Yanga ambapo ilishinda mabao 4-0 dhidi ya CR Belouizdad.
Dube hakusafiri na Azam kwa sababu ni majeruhi ambapo amekosa michezo kadhaa hadi sasa.
Nyota huyo hajacheza mechi ya Azam FC tangu Februari 19 alipoingia kipindi cha pili dhidi ya Tabora United.
Hakusafiri na timu katika mechi mbili za mikoani Mbeya dhidi ya Prisons na Mwanza dhidi ya Singida.
Lakini inafahamika kuwa, kwa kawaida Azam FC husafiri na wachezaji wake hata kama ni majeruhi kama sehemu ya kujenga umoja.
Hata hivyo Dube hakusafiri ikisemekana alikataa kusafiri kama sehemu ya shinikizo ili aachwe huru.
Habari za ndani ni kwamba kuna mfanyakazi mmoja wa Yanga ambaye hapo kabla alikuwa Azam ndiye anayechora ramani ya Dube kuhamia Yanga na klabu hiyo ina uhakika kwamba ishu itakwenda kirahisi kwani staa huyo ameshaanza ‘kuingia kwenye mfumo’ na hadi sasa ametuma barua rasmi ya kuvunja mkataba.
Yanga wanaamini kuwa, wakiipata saini ya Dube watalkuwa wametibu tatizo la namba tisa kwenye kikosi chao hasa ikikumbukwa kuwa tangu aondoke mshambuliaji wao, Fiston Mayele, Wananchi bado hawajapata mshambuliaji wa kuziba pengo lake.
Walianza na Hafizi Konkoni raia wa Ghana lakini mwisho wa siku wakampeleka kwa mkopo Libya, kwa sasa wamemleta Joseph Guede raia wa Ivory Coast, lakini bado hawajamkubali kivile licha ya kuifungia m=timu yake mabao 3 katika michezo nane aliyocheza.
Wananchi wanaamini Dube ndiye mrithi sahihi wa Mzee wa Kutetema aliyewapa raha mitaa ya Twiga na Jangwani kwa miaka miwili mfululizo akirejesha makombe waliyokuwa wameyapoteza Yanga kwa miaka minne.
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPAz
Post a Comment