Taarifa kutoka chanzo cha ndani kimethibitisha kuwa, Klabu ya Azam imefanya mchakato wa wa kutaka kuinasa saini ya beki wa kati wa Yanga SC, Ibrahim Hamad Bacca ili awe sehemu ya kikosi chao msimu ujao.
Chanzo hicho kimeeleza kuwa, licha ya matajiri hao wa Dar kumwekea mkwanja mrefu afande huyo, lakini ameonesha msimamo wake na kugoma kuzungumza na klabu hiyo kwakuwa yeye ni muajiriwa Yanga.
Bacca amesema ana mkataba na Yanga na anafuraha kuendelea kusalia Yanga kwa kuwa maslahi atakayo na mataji ni sehemu ya maisha yao.
Hii inakuja ikiwa ni siku chache baada ya mshambuliaji wa Azam FC, Prince Dube kutangaza kuondoka ndani ya klabu hiyo akidai kuwa haina malengo na kubeba mataji huku akihusishwa kujiunga na Wananchi wa Jangwani 'Yanga SC'.
Itakumbukwa kuwa, mapema Novemba mwaka jana, 2023, Bacca, alisaini mkataba wa miaka minne kuendelea kuitumikia timu ya Yanga SC hadi mwaka 2027.
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPA
Post a Comment