Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema kuwa beki kisiki wa timu hiyo, Henock Inonga ameumia hivyo ameachwa kwenye msafara wa kikosi hicho ambao umeelekea Tanga kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Coastal Union.
Ahmed amesema hayo mara baada ya kutua Tanga kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Coastal utakapigwa kesho katika Dimba la Mkwakwani.
Inonga aliumia enka juzi Machi 6, 2024 kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons uliopigwa katika Dimba la CCM Jamhuri huku Mnyama akipoteza mchezo huo kwa kipigo cha bao 2-1.
"Inonga ameumia na hatujaja naye Tanga, maana yake ni kwamba anakwenda kufanyiwa vipimo zaidi ili kujua nini kimempa shida zaidi ili aanze matibabu. Inonga anatokea Morogoro na kwenda moja kwa moja Dr es Salaam kwa ajili ya matibabu zaidi," amesema Ahmed.
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPA
Post a Comment