Droo ya mechi za Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa 2023/24 imepangwa jana huko nchini Misri.
Wawakilishi wa Tanzania kunako michuano hiyo wamepewa vigogo haswa, Simba wakipangwa na Al Ahly huku Yanga wakipangwa na timu tishio kwa sasa barani Afrika Mamelodi sundowns.
Kitendo cha Yanga kupangwa na Mamelodi kimeonekana kuwafurahisha Mashabiki wengi wa Simba huku waiidhihaki Yanga kuwa hiyo ndio Klabu Bingwa hivyo wajaribu kuona kile ambacho Simba amekuwa akikumbana nacho kwa misimu minne mfululizo.
Simba wao hofu yao sio kubwa kwa kuwa Al Ahly wamekuwa wakikutana nae mara kwa mara na wanahisi wana uwezo wa kufanya lolote.
Sasa Shabiki wa Simba KevSinja 5, kupitia ukurasa wake wa X ameandika;
Yanga wamekua bora sana! kiasi kwamba Simba tunapata amani yeye kupewa Mamelodi. Maana tunajua ndo timu inayoweza kuwazuia kwa sasa!
Simba hatuwawezi Ahly.. lakini simba wamepata amani kujua kua Yanga hawezi fuzu pia!..
Ni aibu kwetu, tulifika mbali zaidi ya hapa!
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPA
Post a Comment