Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Hemed Suleiman Morocco ametangaza kikosi chake kitakachokwenda nchini Azerbaijan kwaajili ya Michezo ya FIFA Series 2024.
Katika kikosi hiki aliyekosekana ni Mbwana Samatta, Dickson Job, Mzamiru Yassin na Metacha Mnata ambao walikuwepo kwenye kikosi kilichocheza AFCON 2023 Ivory Coast mwezi januari, ongezeko ni Clement Mzize na Yahya Zaydi.
Mwingine nani ameongezwa au kupunguzwa?
Michezo hiyo ya kirafiki itahusisha timu 20 kutoka mashirikisho yote sita ya FIFA ambapo kutakuwa na makundi matano na kila kundi litakuwa na timu nne.
Katika Timu nne hizo kwenye kila kundi, kila timu itacheza mechi mbili (itacheza na wapinzani wawili tu badala ya watatu) na hakutakuwa na Bingwa kwa sababu ni mechi za kirafiki za FIFA.
Kundi la Algeria
Algeria - CAF
Andorra - UEFA
Bolivia - CONMEBOL
South Africa - CAF
Kundi la Azerbaijan
Azerbaijan - UEFA
Bulgaria - UEFA
Mongolia - AFC
Tanzania - CAF
Kundi la Saudi Arabia A
Cambodia AFC
Cape Verde - CAF
Equatorial Guinea - CAF
Guyana - CONCACAF
Kundi la Saudi Arabia B
Bermuda - CONCACAF
Brunei - AFC
Guinea - CAF
Vanuatu - OFC
Kundi la Sri Lanka
Bhutan AFC
Central African Republic - CAF
Papua New Guinea - OFC
Sri Lanka - AFC.
Katika Kundi la Azerbaijan ambalo Tanzania yupo, mechi zitapigwa huko Baku kuanzia machi 22 na 25, 2024.
Machi 22, 2024: Bulgaria v Tanzania - Dimba la Dalga Arena, Baku
Machi 22, 2024: Azerbaijan v Mongolia - Dimba la Tofiq Bahramov
Machi 25, 2024: Tanzania v Mongolia - Dimba la Dalga Arena, Baku
Machi 25, 2024: Azerbaijan v Bulgaria - Dimba la Tofiq Bahramov Republican Stadium, Baku.
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPAz
Post a Comment