Klabu ya Azam imethibitisha kupokea barua ya mshambuliaji wao Rais wa Zimbabwe, Prince Mpumelelo Dube (27) akiomba kuondoka kwenye klabu hiyo.
Taarifa ya klabu inasema Azam FC wamemjibu na kumwambia anaweza kuondoka ila kwa kufikiwa kwa vipengele vya mkataba, yaani kama klabu nyingine au yeye mwenyewe anaweza kuilipa Azam FC pesa waliyoweka kwenye mkataba kama mchezaji anataka kuvunja mkataba au timu kumnunua “buy out clause”.
Dube ana mkataba wa miaka 2 na miezi 6 kwenye mkataba wake unaomalizima mwishoni mwa msimu wa 2025/2026.
NYUMA YA PAZIA NINI KINAMUONDOA DUBE AZAM FC
Dube amekuwa akiweka shinikizo la kutaka kuondoka kwa muda mrefu tangu wakati wa Pre-season na kuna klabu ya Kariakoo imekuwa ikimhitaji kwa udi na uvumba baada ya kuondokewa na mfungaji wake mahiri aliyeenda kutafuta malisho kwingineko barani Afrika.
Dube ambaye hayuko pia kwenye mahusiano mazuri na kocha mkuu Yusuf Dabo amekuwa akisumbuliwa sana na simu za Kigogo wa timu hiyo ya Dar es Salaam tangu wakiwa Pre-season na kwakuwa hayuko kwenye mahusiano mazuri na Dabo anaona njia ya kumtia adabu ni kuondoka na kujiunga Kariakoo.
Wachezaji wenzie wamewahi kumsihi asiondoke ili wapambanie ubingwa lakini majibu yake ni viongozi hawamheshimu kwakuwa wameshamzoea kakaa sana na kocha Dabo hawaelewani njia pekee ni kuondoka tu.
Hali ilivyo Azam FC watamgomea Dube msimu huu nadhani baada ya hapo uzoefu unaonyesha watamruhusu aende anakotaka pengine kwa pesa kidogo sana nje ya kile cha kwenye mkataba.
Taarifa zisizo rasmi ni kwamba Dube anataka kwenda timu nyingine ili kutafuta uhakika wa kupata mataji na exposure kwenye kichuano ya Kimataifa tofauti na Azam ambao hawafanyi vizuri sana kwenye Ligi Kuu na hata michuano ya Kimataifa.
Dube ambaye ana miaka 27, anapiga hesabu na kuona mpaka anamaliza mkataba wake Azam atakuwa na umri wa miaka 30, hivyo atakuwa anelekea kwenye uzee kisoka, wapi atapata tena timu kubwa ya kumsajili, majibu ya swali hilo ameona ni bora kuondoka Azam sasa.
Nilizo pewa zinaweza kuwa siyo rasmi ila ni kuwa Dube analalamika juu ya mshahara ambao anapewa na kuibuka kwa wachezaji ambao wanalamba pesa ndefu sana Azam FC, Kama Ahamada, Idrisu, Feisal, Bangala, Dube anataka Mkataba wake uboreshwe na yeye apate kitita kikubwa cha mpunga baada ya kuwa hasikilizwi na mpunga hauongezwi ndipo akaomba kuvunja mkataba.
Waliwahi kuondoka Mrisho Ngassa, Ramadhan Chombo “Ridondo” kwa mtindo kama huu au unaokaribiana, hata usajili wa Salum Abubakar Salum “Sureboy”.
Nadhani Dube na klabu inayomhitaji wanapaswa kuwa na subra kiasi tu, mabosi wa Azam FC huwa hawapendi zogo na timu za Kariakoo analotaka litakuwa ni suala la muda tu.
Ningeshangaa sana watu wakae na Jose au Fredwaaa na Prince yuko Chamazi? Lazima tu ingekuwa hivi katika hali ya kawaida LAZIMA. Mwenye Kisu kikali atakula nyama.
Lakini pia wachezaji wanapenda kucheza mashindano makubwa ya Afrika na kufika mbali, wanapenda kushinda vikombe vya ligi pia. Kwa hiyo wanashawishika kirahisi kwakuwa Kariakoo wanafanikiwa.
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPAz
Post a Comment